SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA ELIMU, YAIPONGEZA TENMET KWA KUANDAA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UBORA WA ELIMU
Naibu katibu mkuu wizara ya Elimu, Dokta Franklin Rwezimula akifafanua jambo wakat wa ufungaji wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu liloandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya (TENMET) Bi. Faraja Nyarandu akielezea lengo la kuandaa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu liloandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania TENMET, Bwana Ochola Wayoga akizungumza wakat wa ufungaji wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu liloandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) jijini Dar es salaam.
Dar es salaam.
Serikali imesema itaendelea kushirikiana wadau wa elimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa inaboresha mazingira na ubora wa Elimu nchini.
Akizungumza wakati akifunga Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu liloandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) Naibu katibu mkuu wizara ya Elimu, Dokta Franklin Rwezimula amesema serikali inatambua na kuunga mkono na juhudi za wadau wa sekta ya elimu nchini.
"Serikali inatambua na kuhunga mkono jitahada zote za wadau mabazo zinalenga kuboresha mazingira ya upatikanaji na kuboresha mazingira ya elimu nchini" Alisema Dkt. Rwezimula
Alisema katika kuhakikisha kuwa hitihada hizo zinafanikiwa nchini serikali imekuwa ikipitia na kuboresha sera na mazingira ya Elimu nchini kwa kuboresha mazingira ya Elimu, kuwapaya mara kwa mara walimu hili kiendana na mabadiliko ya teknolojia
"Lemgo la serikali ni kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa nchini ni bora na inamkomboa mtoto wa Kitanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama TENMET kupitia kongamano hili ambalo linatoa chachu ya kufanya madiliko mbalimbali katika sekta ya elimu nchini" Alisema Dkt Rwezimula.
Nae Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania TENMET, Bwana Ochola Wayoga Amesema katika siku tatu za kongamano hilo wameweza kujadili kwa kina maswala ya Elimu ikiwemo kujadili kuhusu maeneo ya kujifunzia, nyenzo za kufundishia, kujifunza kwa njia za digital, changamoto za mimba za utotoni, mitaala na sera ya elimu.
Ameongeza kuwa katika majadiliano yao wameweza kubainisha kuwa kunahitajika kuongeza kasi ya utoaji wa mafunzo mbalimbali ya mara kwa mara kwa walimu ili kuhakikisha elimu wanayowapa wanafunzi inakidhi matakwa ya elimu bora ikiwa ni pamoja na kuwa na mitaala yenye kukidhi matakwa ya Dunia ya sasa na kutoa mawanda mapana ya mtoto kujifunza kidigital na kupewa nafasi ya kuonesha ujuzi na kipawa chake nje ya elimu ya darasani.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya (TENMET) Bi. Faraja Nyarandu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano ilioutokwa kwa wadau wote wa elimu na Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
"Sisi kama TENMET kipaumbele chetu kikubwa ni kuendelea kuhakikisha kiwa Tanzania na Afrika kwa ujumla inakuwa na Elimu bora kulingana na Kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda Dunia" Alisema Bi faraja.








