Breaking News

WIKI YA USHINDANI YAZINDULIWA, FCC KUTOA ELIMU KWA WADAU JUU YA SHERIA ZINAZOSIMAMIA USHINDANI

Mkurugenzi mkuu wa FCC, bwana William Erio Akifafanua jambo katika mkutano na waandshi wa habari juu ya shughuli ambazo zitafanyika katika maadhimisho ya wiki ya ushindani duniani itakayoanza rasmi November 30 hadi 5 December jijini Dar es salaam. 

Dar es salaam
Tume ya ushindani nchini (FCC) imezindua rasmi wa maadhimisho ya wiki ya ushindani duniani kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali juu ya athari ya upangaji wa njama hususani katika bei za bidhaa jambo ambalo linaloweza kufifisha ushindani katika soko.

Akizungumza jijini Dar es salaam mkurugenzi mkuu wa FCC, Bwana William Erio amesema katika wiki hiyo ya ushindani shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo semina kwa wadau kwa lengo la kukumbushana juu sheria zinazosimamia maswala ya ushindani nchini.

"Katika wiki hii ya ushindani itatumika kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo radio, kukutana na wadau na kufanya semina na wenye viwanda na wafanyabiashara kwa lengo kukumbushana juu ya ushindani wa biashara na nchini" Alisema Bw. Erio.

Alisema katika wiki hiyo pia wadau mbalimbali watapatiwa elimu kwa lengo kuwajengea uwezo na kutambua viashiria vya uwepo wa bidhaa bandia na athari za kiuchumi kwa mlaji.

Ametaja kanda ambazo wadau watafikiwa na kuwa na semina ni kanda ya ziwa ambapo watakutana na wachimbaji wadogo wa madini mkoani shinyanga, kanda ya kaskazini wazalishaji na wasambazaji wa mbegu mkoani Arusha. Wakamuaji wa mchuzi wa zabibu unaotumika kutengeneza   wine na juisi.

Ametaja wengine kuwa ni wadau wa mafuta ya alizeti mkoani kigoma na wafanyabiashara wenye viwanda nyanda za juu kusini mkoani mbeya.

Maadhimisho ya wiki ya ushindani duniani inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 30 November hadi 5 desemba kufikia kilele ambapo siku ya kilele mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa viawanda Dokta Aisha Kijaji na mwaka huu imebeba kaulimbiu ya "Njama za baina ya ushindani na madhara yake kwa walaji na watumiaji"