Breaking News

KAMATI YA SIASA MKOA WA DAR ES SALAAM YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA BARABARA YA TARURA

Dar es salaam
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa Dar es salaam Kundi A wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Abbasi Mtemvu wamefanya ziara ya kukagua miradi ya barabara inayoratibiwa na wakala wa barabara chini ya TARURA.

Wajumbe hao wametembelea na kufanya Ukuguzi barabara ya Goba - kinzudi na barabara ya Jamirex Mwenge ambazo zimejengwa kwa kiwango cha kiwango cha Lami.

Katika ziara hiyo mhe mtevu aliongozana na Mwenyekiti wa (UWT) na Wazazi mkoa Khadija Said na Mwajabu Mbwambo.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo kamati hiyo imetoa pongezi kwa Rais Dkt Samia kwa kutoa fedha na miongozo katika kuboresha miundo mbinu ya barabara kwa falsafa ya Tujenge pamoja. Kwa kushirikisha halmashauri na wananchi katika makazi yao.

"Kamati imeridhishwa na ujenzi wa mradi huu na tunatoa pongezi kwa rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutenga bajeti ya kuhakikisha miradi yote inafanyika na kukamilika kwa wakati hususani miundombinu ya barabara" Alisema Mhe Mtevu.