RC CHALAMILA AUNGANA NA KAMPUNI YA SIMU HALOTEL KUFANYA USAFI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila akishiriki kufanya usafi katika soko la makumbusho zoezi liloandaliwa kwa ushirikiano kati ya Halotel na diwani wa kata ya kijitonyama ikiwa ni sehemu ya kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kuunga mkono jitahada za kuweka Jiji la dar es salaam katika hali ya usafi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi zoezi liloandaliwa na Halotel kwa kushirikiana na ofisi ya Diwani wa kata ya Kijitonyama katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka
Mkurugenzi wa sekta ya biashara Halotel, bw. Abdullah Salum Akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika soko la Makumbusho katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kushirikiana na ofisi ya Diwani wa kata ya Kijitonyama na wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Albert
Picha mbalimbali za zoezi la kufanya usafi katika soko la makumbusho zoezi liloandaliwa kwa ushirikiano kati ya Halotel na diwani wa kata ya kijitonyama ikiwa ni sehemu ya kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kuunga mkono jitahada za kuweka Jiji la dar es salaam katika hali ya usafi
Dar es Salaam:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameungana na kampuni ya simu Halotel kufanya usafi katika Soko la Makumbusho Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila ameshiriki usafi wa pamoja na wafanyabishara wa soko hilo leo Desemba 23, 2023 na kisha alipata wasaa wa kuzungumza na wafanyabishara wa soko hilo.
Akizungumza katika Soko hilo RC Chalamila ameagiza kila jumamosi katika masoko yote ya Mkoa huo kuanzia sasa kila jumamosi ya wiki ufanyike usafi wa pamoja ambapo ameelekeza usafi ufanyike mapema ili kutoa fursa ya biashara kuendelea.
Rc Chalamila ameipongeza Kampuni ya simu ya Halotel pamoja na kutoa huduma bora za mawasiliano nchini kwa kuona umuhimu wa kushiriki kufanya usafi na kutoa msaada vifaa vya kufanyia usafi ambavyo vitawekwa katika soko hilo ambavyo vitasaidia kuweka mazingira safi hivyo kujikinga na milipuko ya magonjwa ambayo gharama yake ni kubwa sana
Aidha RC Chalamila amewashukuru viongozi wa Wilaya ya Kinondoni akiwemo Mhe Mbunge Abas Tarimba, Mstahiki Meya, Katibu Tawala wa Wilaya, Diwani wa Kata ya Makumbusho na wafanyabishara wote pamoja na Watu wengine walioshiriki kwa wingi katika zoezi hilo.
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anawapenda sana ni ukweli usiopingika kila mmoja wetu anaona dhamira yake kwa Taifa nitoe rai kuendelea kumuunga mkono.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa sekta ya biashara Halotel, bwana Abdullah Salum amesema katika kuhakikisha wanasaidia jamii na kuunga mkono harakati za upambanaji leo tijumuika kufanya usafi wa soko la makumbusho na kutoa msaada wa vifaa vya usafi vitakavyosaidia kuweka mazingira yao ya biashara katika hali ya usafi.
"Tunatambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sehemu kama hii ya soko lenye mkusanyiko mkubwa wa watu kukiwa na vifaa vya kusafishia na kuhifadhi taka kama fagio, reki na dustibin kutasaidia kupunguza kuzagaa hovyo kwa taka katika eneo la soko" Alisema Bw. Salum.
Kampuni ya Halotel pamoja na kutoa huduma ya kusambaza mawasiliano zenye ubora wa hali ya juu nchini pia imekuwa mstari wa mbele kutoa misaada kwa jamii hususani katika sekta ya Afya na elimu ikiwa ni moja ya kipaumbelecha kampuni katika kusaidia maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.










