SHEIKH JALALA ASHIRIKI IBADA TAKATIFU YA SIKUKUU KRISIMASI, AIMIZA AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO
kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala akiopokea cheti cha shukrani kutoka kwa mchungaji Leonard Ntibanyike kwa kutambua mchango wake katika kuenzi amani umoja na ushirikiano uliopo nchini katika ibada iliyofanyika katika kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu Jijini Dar es salaam.
kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala akizungumza katika ibada ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo iliyofanyika katika kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu Jijini Dar es salaam.
Mratibu Taasisi sambaza Upendo na Amani, Mchungaji Banza Ikomba akizungumza katika ibada ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo iliyofanyika katika kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu Jijini Dar es salaam.
Dar es Salaam
Jamii imetakiwa kuendelea kuilinda na kuitunza tunu ya Amani, Umoja na mshikamano uliopo hili kuweza kuendelea kuwa na tunu hii adhumu nchini
Akizungumza katika ibada ya kuashimisha misa takatifu ya sikuku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa dini ya kikristo dunia (Yesu kristo) iliyofanyika katika kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu, kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala amesema kwa mujibu wa vitabu vyote vitakatifu Quran na biblia vinatuagiza kuwa na upendo baina yetu wanadamu kwa kutenda mema ambayo hata sisi tungependa kutendewa.
"Vitabu vitakatifu vinatufundisha kuwa na upendo kwa wanadamu wenzetu kwani palipo na upendo ni zao la amani, umoja na mshikamano na ndio maana Leo tunajumuika pamoja kuadhimisha na kusherekea pamoja sikuku hii ya krisimasi bila kujali madhehebu yetu" Alisema Sheikh Jalala.
Alisema tunu hii adhimu ya Amani, Umoja na mshikamano ambayo mwenyezi Mungu ametujalia ndio kila kitu hivyo tuitinze na kuienzi kwani kupitia tunu hii ndio maana leo hii tumekusanyika mahali hapa na kusherekea sikukuu hii kwa pamoja.
Sheikh Jalala aliongeza kuwa kwa mujibu wa mafundisho upendo ndio msingi mkubwa wa dini ya mwenyezi Mungu kwani bila kiwa na upendo hakuna utii kamahakuna upendo basi hakuna amani hivyo amani na upendo ndio kila kitu na neema kubwa Mungu kwa waislam, wakristo na wasio na dini.
"Amani na upendo kati yetu ndio kila kitu na ndipo ilipo neema ya Mungu kwa waislam, wakristo na wasio na dini na ndio maana leo tumeweza kukutana pamoja na kusherekea sikukuu hii ya krisimasi" Alisema Sheikh Jalala.
Aidha Sheikh Jalala amewataka pia viongozi wa dini kuendelea kufundisha watu wapendane na kuishi pamoja kwa ushirikiano kwani hapa maandiko vitabu vitakatifu vinafundisha kuwa kitu kimoja kwani umoja ni asili yetu kwani Baba na Mama wa imani zetu wanadhililisha hilo sisi ni wamoja.
Alisema sisi ni ndugu na undugu wa kwanza ni wa kidini, undugu wa pili wa kuabudu kwani sisi wote tunatoka kwa Mungu mmoja kwa mujibu wa vitabu vitukufu.
Kwa upande wake Mratibu Taasisi sambaza Upendo na Amani Banza Ikomba akiuzungumza katika ibada hiyo ameshukuru kiongozi wa dini ya kiislam dhehebu la Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala kwa kujumuika nao pamoja katika ibada hiyo kwani ni kitendo cha faraja kuona kuwa tukijumuika pamoja kuadhisha sikukuu hii ya krisimasi.
"Kwa dhati kabisa tunatoa pongezi kwa kiongozi wa dini ya kiislam dhehebu la Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala kwa kujumuika nasi katika ibada hii ya kuadhimisha sikuku ya kuzaliwa kwa Yesu kristo kitendo hiki ni cha faraja kubwa kwetu na kinaonyesha kwa jinsi ambavyo tulivyojaaliwa tunu ya Upende kati yetu kama watanzania" Alisema Mchungaji Banda.
Alisema kupitia taasisi ya sambaza upendo na amani tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018 imekuwa mstari wa mbele kufundisha na kutoa mafundisho juu ya kutambua na kuenzi tunu ya Amani, upendo na mshikamano uliopo nchini kwa waumini ya dini zote.
Nae mwenyekiti wa serkali ya mtaa. Wa Gogoni Ally Arobaini akitoa salam katika ibada hiyo amesema anafarijika sana kuona watu wote wanajumuika na kusherehekea pamoja sikukuu hii bila kujali tofauti za imani zao hii linawezekana kutokana na amani na utulivu tulionao nchini.
"Kwa dhati kabisa niwapongeze viongozi wote wa kikristo na kiislam leo mmejumuika pamoja katika ibada hii kusherekea sikukuu ya krisimasi huu ni upendo mkubwa sana hivyo niendele kuwasihihi pia waumini wa madhebu haya na jamii kwa ujumla kuendelea kutunza tunu tulijaaliwa ya amani, umoja na mshikamano " Alisema Bw. Arobaini
kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala akiwa katika ibada ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo iliyofanyika katika kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu Jijini Dar es salaam
Waumini wa Kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu Jijini Dar es salaam wakifatilia mafundisho katika ibada hiyo iliyofanyika kanisani hapo ubungo kibangu Jijini Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania, Sheikh Hemedi Jalala wa (tatu kutoka kulia) akiwa katika Picha ya pamoja na mchungaji Leonard Ntibanyike (tatu kutoka kushoto), mwenyekiti wa serkali ya mtaa. Wa Gogoni Ally Arobaini (katikati) na Mratibu Taasisi sambaza Upendo na Amani Mchungaji Banza Ikomba (wapili kutoka kushoto) mara baada ya misa takatifu ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo iliyofanyika katika kanisa la Goliani Christian church ubungo kibangu Jijini Dar es salaam.











