Breaking News

KADOGOSA:TRILIONI 10 ZIMESHALIPWA KUTEKELEZA MRADI WA RELI YA KISASA (SGR)MIAKA MITATU YA RAIS DKT. SAMIA

Mkurugenzi. wa shirika la Reli nchini Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa ameeleza mafanikio ya reli na Ujenzi wa Miundo mbinu hiyo kupitia miaka mitatu ya Rais Dkt Samia suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha takribani trilion 23.3 ambapo tayari shilingi trilioni 10 zimeshalipwa kutekeleza Mradi huo wa reli ya kisasa.

Hayo yamesemwa. Na Mkurugenzi wa shirika la reli Tanzania Masanja kadogosa alipozungumza na waandishi wa Habari na wahariri wa vyombo vya habari nchini jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa zaidi ya Asilimia 70 ya Bajeti ya serikali imewekeza katika Ujenzi wa Reli ya Umeme (SGR) ambapo Endapo Reli hiyo inaenda kupunguza kero ya uondoaji wa Mizigo kwenda kwenye Bandari kwa kutumia Barabara.

"Reli ya SGR ilianza Awamu ya tatu ya Rais Hayati Benjamin Mkapa, likaanza kutekelezwa na Awamu yatano na kuendelezwa na ya Sita ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan" Amesema Bwana kadogosa.

Aidha kadogosa ametoa wito kwa Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita waweze kushirikiana vyema ili kuboresha miundombinu wezeshi kwa watumiaji huku tayari imeanza kujengwa reli hiyo Kutoka Uvinza mkoani kigoma hadi Msongati.

Wajerumani walikuwa na wazo la kujenga Reli ya (SGR) nchini Tanzania hivyo Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameweza kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu.
"Tuna mpango Madhubuti kufikia Mwezi March 28 Mwaka huu tunapokea vichwa 5 vya treni vya Aina ya Mchongoko mbele kama tulivotoa taarifa hapo Awali " Amesema Bwana Kadogosa.

Serikali yetu imeweza kuingia mkataba wa Ujenzi wa Reli ya (SGR) Tabora hadi Isaka na Benki ya Dunia. Hivyo ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar hadi Makotopola tayari Umeshafikia Asilimia 97.

"Kwa Mwaka fedha 2024/25 tunarajia kuanza wa Ujenzi wa SGR katika Mikoa ya Tanga, Moshi na Arusha.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Shirika hilo,Jamila Mbarouk amesema kuwa tumewaita wanahabari kwenye Mkutano huu Dhumuni kubwa ni kuweza kujenga uelewa kwa wanahabari kuhusu Mradi huu wa kimkakati ambao unaendelea kutekelezwa na serikali yetu.