Breaking News

RAIS SAMIA APIGA SIMU LIVE KATIKA IBADA MAADHIMISHO MIAKA 17 YA KANISA LA WRM

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa Jerry Silaa ambaye alimwakilisha Rais Samia akimkabidhi Prohet Nicolaus Suguye ya pesa taslimu kutoka kwa Rais Samia ajili ya zawadi ya Pasaka kwa Kanisa hilo katika ibada ya kuadhimisha miaka 17 tangu kuanza kwa Huduma za Kiroho ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo Kivule Jijini Dar es salaam April 1, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa simu na mamia ya waumini walioudhilia ibada ya maadhimisha miaka 17 tangu kuanza kwa Huduma za Kiroho Kanisa la WRM ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo Kivule Jijini Dar es salaam April 1, 2024.
Prohet Nicolaus Suguye akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa Jerry Silaa ambaye alimwakilisha Rais Samia katika ibada ya kuadhimisha miaka 17 tangu kuanza kwa Huduma za Kiroho ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo Kivule Jijini Dar es salaam April 1, 2024.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa Jerry Silaa akisalimia mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada ya kuadhimisha miaka 17 tangu kuanza kwa Huduma za Kiroho ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo Kivule Jijini Dar es salaam April 1, 2024.
Baadhi ya mamia ya waumini wa kanisa hilo walioudhulia ibada hiyo ya kuadhimisha miaka 17 tangu kuanza kwa Huduma za Kiroho ibada iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo Kivule Jijini Dar es salaam April 1, 2024.

Dar es salaam:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempigia simu Prohet Nicolaus Suguye katika Maadhimisho ya miaka 17 ya Huduma za Kiroho Katika Kanisa la WRM Kivule Jijini Dar es salaam pamoja na kumpatia pesa taslimu kwa ajili ya zawadi ya Pasaka kwa Kanisa hilo na kuwataka waumini wa kanisa hilo pamoja na watanzania kuyatafakari vyema mafunzo ya dini kwa kuungana na kukaa kwa wema. 

“Wakati nawapongeza kwa kusheherekea pasaka hapo hapo niwatake mtafakari vyema maana ya pasaka lakini pia kuleta ule undugu tunapokusanywa kwenye makanisa kwa umoja wetu basi tukumbe ule undugu na mshikamano kwa umoja “ Alisema Rais Samia. 

Mapema akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Ujenzi Nyumba na maendeleo ya makazi mheshimiwa Jerry Silaa amewaomba waumini na watanzania kwa ujumla waendelee kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan kwa kuendelea kuliongoza Taifa Vyema.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba waumini na viongozi la kanisa kuendelea kumwombea Rais kwani amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuendelea kuliongoza Taifa Vyema na kuletea maendeleo" Alisema Mhe. Silaa. 

Naye Nabii wa Kanisa WRM, Nicolous Suguye akizungumza katika ibaya hiyo ambayo iliudhuliwa na waumini alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia usajili rasmi wa Kanisa hilo.

"Kwa niaba ya watumishi na waumini wa kanisa la WRM kwa dhati kabisa nitoe shukurani zetu kwa mhe Rais Samia kwa kuamua kuridhia na kutoa usajili wa kanisa letu" Alisema Prohet SUNGUYE.