RC CHALAMILA APOKEA NA KUKABIDHI MSAADA KWA WENYE UHITAJI KATIKA KIPINDI CHA RAMADHAN
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 04, 2024 amepokea msaada wa bidhaa mbalimbali kutoka DP world Foundation na kuzikabidhi kwa wenye uhitaji katika Kipindi hiki cha Ramadhan, makabidhiano ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Ilala Boma.
Akipokea msaada huo wenye thamani takribani milioni 200 RC Chalamila amesema mara nyingi akiitwa kupokea msaada huwa hapendi sana kwa sababu baadhi ya watu wanatabia ya kutoa misaada ambayo haina tija sana lakini anaamini msaada uliotolewa leo na DP world Foundation una tija hususani katika mwezi huu wa Ramadhan kwa wakazi wa Dar es Salaam wenye uhitaji ambao wamefunga
Aidha RC Chalamila amesema wanapewa msaada huo sio tu wanauhitaji bali katika mwezi huu wamesimama kuliombea Taifa la Tanzania na Viongozi wake hivyo kila mmoja anawajibu wa kuheshimu imani ya kiisilam. "Ninaimani msaada huo sio sehemu ya CSR ya DP world" Alisema RC Chalamila
Msaada uliotolewa ni mafuta ya kupikia, Sukari, unga wa ngano, mchele, na tende ambapo kwa ujumla wake ni box 50 ikiwa kwa Mkoa huo utapokea box 1000 kila wilaya za Mkoa huo zitapatiwa box 200.







