Breaking News

TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YAANZA KAZI RASMI

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imetoa Matangazo rasmi ya kisheria kwenye Magazeti ya Dailynews na Habari pamoja na Gazetinla Serikali kuhusu kuanza rasmi kwa usajili wa Taasisi za Umma na Binafsi. 

Taasisi za Umma zote zinazokusanya Taarifa Binafsi kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11 ya 2022 zimeshasajiliwana zinatakiwa kukamilisha usajili ili kupata certificate ya kusajiliwa. 

Usajili unafanyika kielekroniki kupitia tovuti ya Tume www.pdpc.go.tz 

Wakati wa uzinduzi wa Tume tarehe 3 Aprili 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza Tume ihakikishe inasajili wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi kabla au ifikapo 30 Disemba 2024.