DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU STANFORD SHAURI LIULI, NYASA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Dayosisi hiyo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Marehemu Askofu Stanford Shauri.
Ibada hiyo inafanyika leo, tarehe 6 Mei 2026, katika eneo la Liuli, Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.







