Breaking News

PROF. MKUMBO SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI, ASIFU UWEKEZAJI WA HEINEKEN

Waziri wa Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa Sekta binafsi nchini hususani katika Uwekezaji hivyo kusaidia kukuza na kuimarika kwa Uchumi.

Akizungumza hafla ya uzinduzi wa muunganiko na ushrikiano kati ya kampuni ya Bia ya Heaken na kampuni ya Namibia utakofahamika kama Heaken Beverage ambayo itahusisha vinywaji vya Vileo zaidi ya viwili katika hafla hiyo iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.
Amesema sekta binafsi imekuwa moja ya sekta ambayo imekuwa na mchango mkubwa nchini hususani katika mapato ya ambapo kwa mujibu wa takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa kampuni hiyo inatoa kodi ya bilioni 11 sasa inakwenda kutoa mapato ya kodi ya Bilioni 21.

"Kwa mujibu wa takwimu kampuni hii inatoa mapato ya kodi ya zaidi ya bilioni 11 ambapo mara baada ya ushirikiano huu kampuni hii inatarajia kuongeza mapato ya kodi mpaka kufikia bilioni 21 hii jambo kubwa na la kupongezwa". Alisema Prof. Kitila. 

Alisema kuwa Sekta binadsi nchini imekuwa kinara katika Uwekezaji ambapo kupitia muunganiko huu utawezesha kutoa fursa zaidi katika maeneo mbalimbali sambasamba na kuongezeka kwa ajira nchini pamoja na biashara.
Aidha Prof kitila aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuweka kutunga sera na kuweka mazingira wezeshi kwa lengo la kuvutia Uwekezaji jambo linalofanya wawekezaji na kampuni za nje kuungana au kushirikiana na kampuni zilizopo nchini kutokana na mazingira mazuri pamoja nqa sera mzuri za Uwekezaji na biashara.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia imejikita katika kueweka mikakati bora ya Uwekezaji ikiwa ni pamoja wadau wote wanaohusika na Uwekezaji kuwa na sauti moja kwenye eneo kuondoa changamoto kwa wanaotaka kuwekeza nchini.
"Nimefurahi kushuhudia uzinduzi wa Ofisi mpya ya Heineken nchini Tanzania. Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji wa Tanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu na kuongeza ajira. Kujikita kwa Heineken kwenye soko letu ni dhahiri, na ninatazamia kuona matokeo chanya ya jalada lao jipya iliyopanuliwa kwa uchumi na watu wetu”. alisema Prof. Kitila.

Nae Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade, amesema Kuunganishwa kwa biashara ni hatua muhimu katika ukuaji wa kampuni nchini na ni kielelezo ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini upanuzi wa kinywaji cha Heineken zaidi ya kinywaji cha bia.
“Inaonyesha ari yetu kutokana na uzoefu wa kipekee kuhudumia watumiaji wa Kitanzania ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji tukidumisha nyakati za umoja wa kweli. Sasa kuna toleo la kinywaji cha Heineken kwa ajili yako kwa chochote unachohitaji. Uzinduzi huu unaashiria sura ya kuvutia kwetu tunapoendelea kukua na kukidhi soko la Tanzania”. Alisema Bw. Fagade

Kwa upende wake Meneja wa Masoko na Biashara bi. Lilian Pascal amesema kuwa Sekta wanakwenda kuongeza ajira kwani idadi iliyokuwepo ilikuwa ya kinywaji kimoja sasa iko zaidi vinywaji viwili.

Amesema muunganiko huo unaenda kuongeza fursa zaidi ikiwemo kuongeza ajira zaidi pamoja na kuongeza mapato hivyo kukuza ulipaji wa kodi.