DC MPOGOLO AWATUNUKU VYETI MADEREVA 1518
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Jonas Mpogolo, amewatunuku vyeti vya uthibitisho madereva 1518 waliofanya mtihani na kuthibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).
Jumla ya wahitimu wa mafunzo na uthibitisho huo ni madereva 2517.
Hafla ya ugawaji vyeti hivyo imefanyika katika Ukumbi wa mikutano Arnaoutoglou ,jijini Dar es Salaam ambapo DC Mpogolo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Albert Chalamila.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo madereva, kamati ya Uthibitishaji wa madereva na Usajili wa wahudumu, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na vyama vya wasafirishaji.
Mpogolo aliwataka madereva hao kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa manufaa yao na abiria, huku akisisitiza madereva ambao hawajsthibitishwa kujitokeza.




