Breaking News

DTK. ABDALLAH: SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMJ JUU YA FAIDA ZA KURASIMISHA BIASHARA

Serikali imesema itaendelea inaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu na faida za kurasimisha biashara ukizingatia urasimishaji wa biashara kwasasa unafanyika kwa njia ya mtandao

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo siku nne kwa waandiahi wa habari wanaoandika habari za biashara Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dokta Hashil Abdallah amesema mafunzo hayo yenye lengo la kuwapatia uelewa sahihi kuhusu shughuli zinazohusu BRELA na namna ya kuziripoti.

Alisema kupitia mafunzo hayo washiriki wataweza kuwa mabalozi na kubeba agenda zitakazoleta mchango  chanya kuhusu urasimishaji wa biashara kubeba agenda chanya ya Brela hususan katika urasimishaji wa biashara itasaidia wananchi kufunguka na kunufaika na Brela katika kukuza uchumi wao binafsi na pato la taifa.

"Kupitia mafunzo haya waandishi wataweza kuwa mabalozi wazuri kwa kubeba agenda chanya ya Brela hususan katika urasimishaji wa biashara itasaidia wananchi kufunguka na kunufaika na Brela katika kukuza uchumi wao binafsi na pato la taifa". Alisema Dkt. Abdallah.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bwana Godfrey Nyaisa amesema lengo ka kuandaa mafunzo haya ni baada ya kuona habari zinazohusu BRELA zina mambo mengi yakiwemo ya kisheria, hivyo ni vema waandishi wa habari tukawajengea uelewa na kuwawezesha kuwa na ufahamu wa kutosha wa kuandika habari zinazohusu taasisi

Alisema kwa kuanzia tumeanza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam hasa wanaondika habari za BRELA lakini mikakati yao ni kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa waandishi wa Mikoa yote na lengo ni kuhakikisha wanaendelea kuwajengea uwezo wadau muhimu wakiwemo waandishi wa habari.

Aidha amesema mpango wa mkakati wa BRELA ni kuwa na kanzi data ya waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika habari za Wakala huo ili kusaidia kuwa na habari zenye usahihi na kwamba mafunzo hayo yanaendelea kutolewa sambamba na kuwaita katika matukio yanayohusu BRELA.

Pia amesema kuanzia sasa wataanza kutoa tuzo Maalum kwa waandishi wa habari za biashara ambao watakuwa wakiandika makala zenye matokeo chanya kwa jamii lakini makala ambazo zitakuwa zimejitosheleza.
"Tutakuwa na tuzo maalum kwa waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika Makala zinazohu BRELA.Tutakuwa tunashindanisha makala hizo na mshindi wa kwanza ambaye atakuwa ameandika makala Bora atapewa tuzo na itakuwa ENDELEVU,"amesema Nyaisa katika mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza kutolewa na Wakala huo 

Kuhusu majukumu ya BRELA ni  pamoja na kusajili Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, Viwanda vidogo, kutoa Hataza, Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda. Menejimenti na Wafanyakazi wa BRELA, wapo tayari kukusikiliza na kutoa huduma bora ili kufanikisha lengo lako.