TAMISEMI KISIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NI KUKIUKA SHERIA: ACT WAZALENDO
Katibu mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado shaibu amesema kwamba Tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI inajivika wajibu ambao ni wa Tume huru ya uchaguzi wa kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu 2024.
“Hiki ambacho TAMISEMI wanaendelea kukifanya kinavunja sheria ya taifa ya uchaguzi kwahiyo basi ni batili na kinyume cha sheria ya nchi yetu na ACT Wazalendo tungependa kusema kwamba uamuzi huu wa TAMISEMI sio tu kwamba ni jambo la hovyo lakini pia ni jambo la kijambazi na wote ambao wapo nyuma ya mchakato huu wanaipeleka Tanzania kwenda katika mkondo wa taifa la kijambazi ambapo moja ya msingi wake ni kutojali kabisa misingi ya sheria na misingi ya katiba kwasababu ni jambo ambalo haliwezekani” amesema Ado
“Wadau wa siasa Tanzania tumepambana tangu uchaguzi wa mwaka 2020 na sisi ACT Wazalendo tulikuwa mstari wa mbele kupigania mageuzi ya kisiasa nchini Tanzania na sheria mpya zikaandikwa, tumeandika sheria ya tume huru ya uchaguzi, sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani na tumefanya maboresho ya sheria ya vyama vya siasa nchini na ilikuwa matarajio ya wadau tunapokwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani hizi sheria mpya ambazo tumeandika ndizo zitakazo enda kufanya kazi lakini kinyume na matarajio ya wadau hivi sasa TAMISEMI inataka kujivika wajibu ambao ni wa Tume huru ya uchaguzi” amesema Ado
Ametoa kauli hiyo Juni 12, 2024 Makao makuu ya Chama hicho Jijini Dar es salaam mara baada ya TAMISEMI kutuma barua kwa Chama hicho kushiriki katika kujadili kanuni zitakazo simamia uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2024, na kuwa wataendela na mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mita




