TCRA: VYOMBO VYA HABARI NI NGUZO MUHIMU YA MAFANIKIO KATIKA MCHAKATO MZIMA KUELEKEA UCHAGUZI
Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada katika semina ya waandishi wa habari kuhusu Wajibu na Majukumu ya Vyombo vya Habari na Utangazaji katika kuelemisha umma katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Patrick Kipangula akifafanua jambo kuhusu maadili ya uandishi wa habari katika wa uchaguzi mafunzo yaliofanyika katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitaka vyombo vya habari nchini kutambua nguvu na ushawishi ulionao katika jamii hususani katika kuelekea kuanza kwa zoezi la Maboresho ya Daftari la Kudumu la Mpinga Kura yatakayozinduliwa Julai 1, 2024 mkoani Kogoma.
Akiwasilisha mapama leo Juni 14, 2024 Meneja Huduma za Utangazaji wa TCRA Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha Mada kuhusu Wajibu na Majukumu ya Vyombo vya Habari na Utangazaji katika kuelemisha umma katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yaliyoratibiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
"Kama TCRA tunaendelea kuhakikisha wanahabari wanafanya kazi katika mazingira rafiki kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuelekea maboresho ya Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. Vyombo vya habari vinatakiwa kujua kwamba vinaushawishi mkubwa katika jamii. Asilimia 40 ya mwenendo wa jamii imechangiwa na vyombo vya habari," amesema Mhandishi Kisaka na kuongeza,
"Hivyo sisi (vyombo vya habari) tunao wajibu mkubwa wa kuitengeneza jamii na kuifanya kuwa bora, hivyo tujue tuna ushawishi mkubwa, tuelewe tunapokwenda kutoa taarifa, tujue tunakwenda kushawishi watoto na vijana. Tujitambue kwamba tunaushawishi mkubwa katika jamii,".
Mhandisi Kisaka ameongeza kuwa vyombo vya habari vinatakiwa kutambua kuwa vinahusika katika kuiunganisha jamii katika maendeleo ambapo amevitaka kujua vinajukumu la kuileta jamii pamoja na kuchochea maendeleo.
Akizungumzia kuhusu takwimu za vyombo vya habari vya utangazaji nchini, amesema Redio ni chombo cha kwanza chenye nguvu kinachofikia wananchi wengi, kwamba yeyote atakayetumia Redio ajue anawafikia watu wengi kuliko kitu chochote.
Mhandishi Kisaka amesema watu wengi huweza kusikiliza matangazo kupitia Redio kwa vile huweza kuendelea kufanya shughuli nyingine za kiuchumihuku wakisikiliza matangazo kupitia Redio.
"Hivi sasa matangazo kwa njia ya Redio nchini (Fm) yanafikia asilimia 76 ya watu," ameeleza Mhandisi Kisaka.
Kwa upande wa utangazaji kwa njia ya Televisheni, Mhandisi Kisaka amesema utangazaji kwa njia ya Televisheni hupendwa na watu wengi kwa sababu ya kuweza kusikia pamoja na kuona mwenendo wa matukio yanayoendelea.
Hata hivyo ameeleza kuwa tofauti na Redio, bei za 'receivers' ni kubwa, hivyo kufanya watu wachache kumiliki 'TV Sets' ambapo idadi ya watu wanaofikiwa na utangazaji wa Televisheni kwa njia ya Satellite (DTH) ni asilimia 100.
Mhandisi Kisaka amebainisha kuwa vyombo vya habari vya utangazaji ni nguzo muhimu ya mafaikio katika mchakato mzima wa kuelekea uchaguzi.






