Breaking News

ELVA SABAYA AIBUKA MSHINDI MISS ILALA 2024

Miss Elva Sabaya mara baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Ilala 2024 katika ukumbi wa Warehouse Arena jijini Dar es salaam.
Miss Ilala 2024 Elva Sabaya
Miss Ilala 2024 Elva Sabaya akiwa na mshindi wa pili Olivia Laswai na mshindi wa tatu Zena Meremo mashindano yaliofanyika katika ukumbi wa Warehouse Arena jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Mrembo Elva Sabaya mwenye umri wa miaka 21 amefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza kuwashinda warembo wengine 13 na hivyo kutangazwa rasmi kuwa mshindi wa Miss ilala kwa mwaka 2024.

Akizungumza wakati akiwatangaza washindi wa shindano Miss Ilala 2024, Chief judge Deogratius Kitama amesema mashindano ya mwaka huu yameboreshwa sana na kuwa na viwango vya hali ya juu kwa lengo wa kupata washindi ambao wataenda kufanya vizuri katika ngazi ya taifa ( Miss Tanzania) 

"Mashindano ya mwaka huu 2024 tumeyaboresha zaidi hili kuweza kupata warembo ambao wataenda kutoa washindi katika nafasi za juu katika ngazi ya kitaifa ( Miss Tanzania) 2024 kwa kuchagua warembo wenye viwango vizuri". Alisema Chief judge Deogratius Kitama 

Awali akiwataja washindi wengine waliofaniliwa kuingia tatu bora kuwa ni Olivia Laswai umri wa miaka 22 aliyeshika nafasi ya pili na Zena Meremo miaka 21 ambae ameibuka mshindi wa tatu.

Warembo hao walipita jukwaani kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali ikiwemo vazi la utamaduni, ufukweni, na ubunifu ambapo mshindi wa kwanza Elva Sabaya alipata zawadi ya fedha laki 5, mshindi wa Pili Olivia Laswai laki 4 na mshindi wa Tatu Zena Meremo akiambulia laki 3.

Mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Warehouse Arena usiku wa Agoust 16 jijini Dar es salaam