MCHUNGAJI MASHIMO: TUTAKATA RUFAA KUPINGA KUFUNGIWA KWA KANISA LA KIBOKO YA WACHAWI
Mchungaji wa Taifa, Nabii Nikaya Komando Mashimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua zilizochukiliwa mara baada ya kufungiwa Kanisa la Kiboko ya Wachawi ya mapema leo Agoust 2, 2024 jijini Dar es salaam.
Mchungaji Anna Gidion Nsanza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu kufungiwa Kanisa la Kiboko ya Wachawi ya mapema leo Agoust 2, 2024 jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Mchungaji wa Taifa, Nabii Nikaya Komando Mashimo amesema tayali ameshawasiliana na mwanasheria kuanza mchakato wa kukata rufaa kupinga hatua ya seikali kulifunga Kanisa la Kiboko ya Wachawi.
Akizungumza mapema leo Agosti 2, 2024 Kanisa hapo Buza jijini Dar es Salaam amesema hatua hiyo sio kwamba wanaipinga serikali juu ya hatua ya kulifunga kanisa hilo bali ni kumtaka msajili kubainisha na kuweka wazi chanzo cha kufungiw kutoa huduma au kuweka wazi kama kuna changamoto nyingine tofauti na iliyoelezwa kuwa mchungaji huyo amefungiwa kutokana na kutoza fedha waumini ili kupata huduma.
"Ndugu zangu eaandishi wa habari mnaowaona hapa ni wahimini wa kanisa hili mkipata mda fatilieni juu ya Huduma ambayo imekuwa ikitolewa na madai yaliyotumika kufungia huduma ni kweli. Hapa huduma inalayotolewa na kuponya waumini wengi sambamba na kubadilisha maisha ya watu waumini wamekuwa wakihudumiwa bure, hivyo ombi letu ni kuiomba Serikali kuangalia upya jambo hili,".Alisema Mchungaji Mashimo.
Pia ametoa wito wananchi na wadau wengine wasihusishe kufungiwa kwa kanisa hilo na Serikali, kama maana iliyofungia taasisi.
Kwa upande wake Pasta Anna Sunza akizungumzia sakata hilo amesema tangu amefika katika kanisa hilo amepona maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakimkabiri kwa kipindi kirefu.
Alisema amesikitishwa na kuumizwa sana na kauli ya kuwa kuwa Mchungaji wao ni tapeli kama ambayo inasemwa na vumishwa na baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mtandao ya kijamii.
"Kwa kipindi kirwfu nikuwa nikisumbuliwa na tatizo la moyo lakini mara baada ya kufika kanisani hapo na kuombewa amepona kabisa tatizo hilo hivyo napenda kuwasihi wananchi wenzangu kuouuza taarifa kuwa mchungaji huyo ni tapeli". Alisema Bi. Sunza.
Nae mmoja ya waumini wa kanisa hilo ambaye anajishugulisha na biashara ya kuuza chakula 'Mama Ntilie' pembezoni mwa kanisa Hilo, Bi Shukrani Ismaeli amesema uwepo wa Kanisa Hilo umesaidia kupunguza vitendo vya uhalifu ukiwemo wizi, utumiaji wa dawa kulevya, ukabaji.
"Kwa kweli wizi ulikuwa umepungua Sana, sasa sijui hali itakuwaje baada ya kufungiwa kwa kanisa, hivyo naomba Serikali iangalie kwa huruma, ila Luna mengine waweke wazi,". Alisema Bi Ismael.







