MKUTANO MKUU WA KWANZA WA MFUKO WA MFUKO WA WATUMISHI HOUSING INVESTMENT KUFANYIKA AGOUST 10 JIJINI DAR
Na Neema Mpaka:
Mfuko wa Watumishi Housing Investments (WHI) unataraji kufanya Mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa Uwekezaji na faida (Faida Fund) Agoust 10 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere (JNCC) jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa (WHI), Dokta Fred Msemwa amesema mkutano huu wa kwanza tangu kuasisiwa kwa mfuko huo umelenga kutoa fursa kwa wawekezaji wote wa mfuko kupokea taarifa za mwenendo wa mfuko.
"Katika mkutano huu washiriki watapata wasaa wa kupokea taarifa ya fedha ya mfuko ya mwaka unoishia Juni 30,2024 pamoja na maendeleo na mipango ya mfuko katika kipindi hicho sambamba na fursa za uwekezaji zilizopo" Alisema Bw. Msemwa.
Alisema katika kipindi hicho mfuko umeweza kuweka misingi imara ya ambayo imeweza kumaliza ombwe la wawekezaji wadogo kushindwa kushiriki katika uwekezaji hususani katika masoko ya fedha nchini.
Aidha bwana Msemwa aliongeza kuwa mkutano mkuu wa kwanza unafanyika kwa kuzingatia sheria ya mamlaka ya masoko na mitaji (CMSA) ambazo zinawataka kufanyika kwa mkutano huo kila mwaka.




