WATUMISHI WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA.
Na Mariam Muhando - Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalum anaewakilisha Wafanyakazi Dokta Alice Kaijage amewatakata watumishi kujitokeza katika Zoezi la Uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili waweze kuchagua Viongozi Bora.
Dkt. Kaijage ameyabainisha hayo leo Agoust 6, 2024 mara baada ya kufanya Ziara Jijini Dar es salaam yenye lengo la Kusikiliza kero za Watumishi na kuzipatia Ufumbuzi sambamba na kuyaeleza mambo mema aliyoyafanya Rais Dokta Samia Suluhu Hassani katika kuwaleta Maendeleo.
Amesema Nchi inaelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo Watumishi ni sehemu ya Taifa kwani kila mtanzania anaowajibu wa kupiga kura hivyo Rais Samia amewakumbuka katika kuwaletea maslahi Bora.
"Kwa mujibu wa Katiba yetu ibara ya tano inaelekeza ni wajibu wa Watumishi kupiga kura wasipo jitokeza katika zoezi hilo hawatoweza kupiga kura na kupata Viongozi Bora hivyo naawahidi yale yote mlioyapendekeza nitakwenda kuyafanyia kazi Kwa kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia ni Sikivu na inakwenda kusimamia maslahi bora ya Watumishi ".Alisema Dkt. Kaijage.
Katika hatua nyingine Dkt. Kaijage amewashukuru Viongozi mbalimbali wa Mkoa Dar es salaam Kwa mapokezi mazuri Mkoani humo.
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Meya wa Jiji, katibu tawala na Mkurugenzi wa Jiji kwa mapokezi mazuri". Alisema Dkt. Kaijage.
Mapema akizungumza mara baada ya ziara Mkuu wa Divisheni ya Rasilimali Watu na Utawala, bwana Selemani Kateti amempongeza Mbunge anaewakilisha Wafanyakazi kwa hatua yake ya kukutana na Watumishi mbalimbali kwa lengo la kusikiliza na kuzipatia Ufumbuzi changamoto zao.
"Nikuahidi kuwa tutakwenda kuyafanyia kazi yale yotw aliyotuelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo maslahi ya Watumishi,". Alisema Bw. Kateti.






