MSAJILI WA VYAMA AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO CHINI YA TCD, DKT. NCHIMBI, MBOWE, PROF. LIPUMBA, DOTOTHY SEMU NA SELASINI WASHIRIKI
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, akiongoza Kikao cha Mashauriano na Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho, mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kilihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali.
Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 18, 2024 jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Chadema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD kwa sasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu Dorothy Semu, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Ndugu Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi.
Aidha kwa upande wa Serikali pia uliwakilishwa na Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.







