Breaking News

NAIBU SPIKA AWATAKA WAHITIMU WA CHUO CHA FURAHIKA KUWA MABALOZI WAZURI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa jimbo la Ilala mhe. Mussa Zungu akitoa vyeti kwa mmoja ya wahitumu wa mahafali 19 ya chuo cha Ufundi Stadi Furahika kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika, Dokta David Msuya akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa jimbo la Ilala mhe. Mussa Zungu katika mahafali ya 19 ya chuo cha Ufundi Stadi Furahika kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es salaam.
Bahadhi ya wahitimu wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa jimbo la Ilala mhe. Mussa Zungu katika mahafail ya 19 ya chuo hicho yaliofanyika Buguruni Malapa jijini Dar es salaam.

Dar es salaam
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu amewataka wahitimu wa Chuo Cha Ufundi Stadi Furahika kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es salaam kuwa mabalozi wazuri kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujiendeleza kitaaluma zaidi ili waweze kufikia ndoto zao.

Akizungumza katika mahafali ya 19 ya chuo hapo amesema Serikali imekua ikiweka mazingira rafiki kwa kushirikiana na shule na vyuo binafsi ili kuhakikisha watanazania wanapata Elimu itakayowasaidia katika Maisha yao na Taifa kwa ujumla.

"Kwanza niwapongeze kwa kuhitimu mafunzo wote katika kada mbalimbali, jambo ambalo ni muhimu zaidi na msiishie hapo mlipoishia na badala yake mjiendeleze zaidi kitaaluma ili kuweza kushindana katika ushindani wa soko la ajira". Alisema Mhe. Zungu.

Alisema ajira zilizopo aziwezi kutosha kila muhitimu hivyo basi wahitumu mnaohitimu leo kuweni wabunifu na kujituma na nidhamu huko waendako kwani watakuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho, hali hiyo itawasaidia kufanya kazi vizuri nakwa mafanikio makubwa.

Katika hatua nyingine Naibu Spika huyo ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika suala la elimu, kwa kutoa elimu ya fundi kwa vijana bila malipo na kuahidi kusaidia baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo hicho ili kiweze kufanya kazi zake

Awali akizungumza wakati akimkalibisha mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika, Dokta David Msuya ameiomba serikali kusaidia kuchangia vifaa vya kuendeshea Chuo hicho kwani wanatoa elimu bila malipo.

"Tukushukuru sana Naibu Spika na 
kwa kuweza kujumuika nasi katika mahafali haya ya 19 ya chuo chetu pamoja na kuwa na changamoto mbalimbali lakini kimekuwa kikitoa elimu ya ujuzi bure ikiwa ni kuunga mkono serikali inayoongizwa na rais Samia ya kuhakikisha kila mtu anapata fursa ya kupata elimu" Alisema Dkt. Msuya.

Alisema wameamua kutoa elimu ya Ufundi kwa vijana wa kike na kiume ili kusaidia kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya na biashara ya kuuza miili kwa vijana wa watoto wa kike ambayo husababishwa na vijana hao kukosa elimu ambayo huwasaidia kupata ajira au kujiajiri

Aidha Dkt Msuya aliongeza kusema mafunzo yanatolewa bure huku ambapo kila mwanafunzi atachangia shilingi elfu hamsini pekee kwa ajili ya mitihani tu.

Katika mahafali hayo ya 19 jumla ya 45 wamehitimu mafunzo ya stadi za kazi (Ufundi) katika fani mbalimbali huku wahitimu wengi waliohitimu katika Chuo hicho wameajiriwa katika sekta tofauti tofauti hapa nchini.