Breaking News

CUF YATANGAZA RATIBA YA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI KATIKA UCHAGUZI MKUU 2025

Dar es Salaam - Chama cha wananchi (CUF) kimetangaza kuanza rasmi mchakato wa kutoa fomu kwa wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani upande wa jamhuri ya muungano wa Tanzania bara na uchaguzi wa Rais, Wawakilishi na madiwani kwa upande wa Zanzibar unaoatarajiwa kufanyika mwezi ocktoba mwaka huu.

Akizungumza mapema leo April 25, 2025 makao makuu ya chama Buguruni jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Taifa bwana Yusuph Mbugiro amesema zoezi la kuchukua fomu na kurejesha kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar litaanza 15/05/22025 hadi 30/06/2025 na mkutano wa uteuzi wa wagombea utafanyika 27/072025.

Alisema kwa upande wa Ubunge na Uwakilishi zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litaanza 6/06/2025 mpaka 7/07/2025 ambapo kura za maoni zitafanyika kati ya tarehe 11/07/2025 hadi 20/07/2025. Ngazi ya Udiwani zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 20/07/2025.

“Nichukue nafasi hii kuwaomba wanachana na wafuasi wa chama wenye vigezo vya kugombea nafasi tajwa kujitokeza kuchukua fomu wasiyumbishwe na kubabaishwa na maneno ya upotoshaji dhidi ya msimamo wa chama bali tuendelee na harakati zetu za ujenzi wa chama na kupigania ujenzi wa demokrasia ya kweli kwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kushiriki uchaguzi hili kuweza kutimiza lengo kuu la chama kushika mamlaka na dola ya nchi yetu”. Alisema Bw. Mbugiro.

Alisema chama kinajua kwamba bado malalamiko yetu mengi ayajafanyiwa kazi ipasavyo ikiwemo suala la madai ya Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi lakini jambo hili aliwezi kutuzuia kuingia katika uchaguzi kwani kufanya hivyo ni sawa na kumwachia shamba la mihogo nguruwe.

“Chama kimejipanga kuendelea kupigania upatikanaji wa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi mpaka tutakapofanikiwa kwani swala hilo sio kwa maslahi ya chama chetu tu bali kwa maslahi mapana ya ustawi wa taifa na watanzania kwa ujumla”.  Alisema Bw. Mbugiro.

Aidha bw. Mbugiro amewataka viongozi na wanachama kwa ujumla kuendelea kufanya maandalizi ya kutosha kwa kufuata sheria na taratbu za ndani ya chama ikiwemo kuzingatia katiba ya chama na kanuni hili kuhakikisha kuwa tunaingia katika uchaguzi huu kwenda kutoa ushindani mkubwa na kushinda katika ngazi zote.

Katika hatua nyingine Bw. Mbugiro ametoa wito kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan kutumia fursa ya uchaguzi huu kudhibitisha kwa vitendo dhamira yake anayoihubiri muda wote kuwa anahitaji kuona watanzania wanaishi kwa amani na utulivu na kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki kwani hakuna mtu mwenye haki miliki ya taifa letu.

“Dunia nzima inaitazama Tanzania kupitia uchaguzi huu Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo anamtazama mhe. Rais na watanzania na anaona yaliowazi na yaliojificha ndani ya mioyo yetu, hivyo basi ni vyema kwenye uchaguzi huu wote tutizame maslahi ya nchi na watu wake badala ya kuangalia maslahi binafsi au ya vyama vyetu”. Alisema Bw. Mbugiro.

Katika hatua nyingine Bw. Mbugiro ametoa wito kwa wananchi ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha, kubadili au kuhakiki taarifa zao kujitokeza katika awamu hii ya pili inayoanza mwezi Mei 2025 na Tume huru ya  uchaguzi kuwaandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura kwa wananchi ambao wametimiza sifa za kupiga kura.

Pia ameitaka Tume huru ya uchaguzi kutoa mapema Makala ya daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa kama wadau muhimu hili tuweze kupitia na kutoa maoni yetu pamoja na kuliweka wazi hili wananchi waweze kuhakiki taarifa zao na kuweka mapingamizi kwa wale wasiokuwa na sifa ya kuwemo katika daftari hilo.