Breaking News

KHIMJI ATIMIZA AHADI YA KUPELEKA MAJUZUU NA MISAHAFU MADRASSA NURI-LYAQIIN - KATA YA ILALA

Ndugu Said Rajab Dogo Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Ilala kwa kushirikiana na Ndugu Tatu Hassan Haji katibu wa CCM Tawi la Kasulu wamemwakilisha Mhe Saady KhimjiDiwani wa Kata ya Ilala na Mjumbe wa Baraza Kuu la WAZAZI CCM Taifa katika kukabidhi ahadi aliyoahidi baada ya kupatiwa Ombi la uhaba wa Majuzuu na Misahafu katika Madrassatul Nuri - Lyaqiin iliyopo Kata ya Ilala.

Pamoja na kupokea utekelezaji wa ahadi ya Mhe Khimji bado kulikuwa na ombi jipya la kurekebisha baadhi ya eneo linalopitisha maji mvua ikinyesha Madrassatul (Chuoni) hapo.
Akiongea na Wawakilishi wa Diwani Mudihru (Ustaadhi Mkuu wa Madrassa hiyo) Shekhe *Muhidin Shabani Mtambo* alimshukuru Mhe Khimji Diwani kwa kusaidia jambo la heri katika Madrassatul hiyo, sote tunatambua Madrassa ni sehemu muhimu katika jamii kwa ajili ya kuwaandaa watoto kuja kuwa watu wema na Viongozi waadilifu hapa Tanzania. 

"Mwenyezi Mungu amjaalie kila la heri Diwani wetu amfungulie riziki ndogo na kubwa ili aweze kusaidia jamii anayoiongoza, lakini pia kwa kuwa Mhe Khimji amepata changamoto ya Kiafya leo tutamuombea duwa Mwenyezi Mungu ampinye kwa haraka ili aendelee na Majukumu ya Kata yetu ya Ilala" alisema Shekhe Muhidin.

"Endelea na kusoma, na Mola wako Mlezi aliye Karimu kushinda wote, atakutukuza wala hatakudharau".- Surat Al Alaq.
"Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu" - MT 12:35 - 36

ELIMU DUNIA NA ELIMU AHERA NI WAJIBU WETU SOTE.