UJUMBE KUTOKA UN TOURISM WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA
Ujumbe wa Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism ) ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Zurab Pololikashvili, umefanya ziara ya utalii katika Hifadhi ya Taifa Arusha leo Aprili 24, 2025 pembezoni mwa Jukwaa la Pili la Kimataifa la Utalii wa Vyakula la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) kwa Kanda ya Afrika ambapo ulitembelea maporomoko ya maji Tululusia.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) na baadhi ya Watendaji kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) walishiriki katika ziara hiyo.









