VIJANA JITOKEZENI KUHAKIKI NA KUBORESHA TARIFA ZENU KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - JESCA MSHAMA
Dar es salaam - Katibu wa Idara ya Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bi Jesca Mshama, amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika awamu ya pili kuhakiki na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga linalotarajiwa kuanza Mei 1 hadi 7 2025.
Akizungumza mapema leo April 29,2025 jijini Dar es salaami amesema hii ni fursa muhimu kwa vijana kutambua nafasi yao katika mustakabali wa taifa, kwa kuhakikisha wanajiandikisha, kuhakiki na kuboresha taarifa zao ili wapate haki ya msingi ya kupiga kura.
“Nitoe rai kwa vijana kujitokeza kwa wingi awamu hii ya pili kujiandikisha na kuhakiki saarifa zao hili waweze Kupiga kura na kutimiza haki ya msingi na sauti ya mabadiliko kwani ni hatua muhimu ya kidemokrasia,” Alisisitiza Bi Mshama.
Alisema kwa mujibu wa taarifa iliyoyolewa na na tume huru ya uchaguzi mchakato huo awamu ya kwanza inayoanza Mei 1, 2025 utaanza katika mikoa ya Geita, Mwanza, Ruvuma, Mbeya na Songwe.
Ambapo awamu ya pili itakayoanza Mei 16 hadi 22, 2025 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro.
Aidha, Mshana aliwataka vijana wajitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, akisisitiza kuwa taifa linahitaji fikra mpya na uongozi wenye dira kutoka kwa vijana.
“Tunahitaji mawazo mapya, Vijana waonesheni uwezo wenu kwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ili kubeba ajenda za maendeleo kwa vizazi vya sasa na vijavyo,” Alisema na kuongeza kuwa
"Niwakumbusha vijana kuwa uvivu wa kushiriki mchakato wa uchaguzi huacha nafasi kwa watu wasiokuwa na dhamira njema kuongoza taifa ni kuruhusu mustakabali wenu kuamuliwa na wengine,”.
Katika hatua nyingine, Jesca Mshana amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na mshikamano uliopo nchini akisema umoja wa vijana a chama cha mapinduzi hawatakubali kuona amani ya nchi inavurugwa.
“Tunaamini katika misingi imara ya waasisi wa taifa hili, na viongozi wa sasa wanaendeleza hilo. Amani ni urithi wetu, na vijana tuna jukumu la kuilinda kwa gharama yoyote,”. Alisema Bi Mshama
Zoezi hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaingia awamu ya pili uboreshaji utaendelea katika vyuo vya elimu ya juu pamoja na vituo vya magereza ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.




