RAIS SAMIA KUKUTANA NA VYAMA VYA SIASA KUPOKEA ILANI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa atakutana na vyama vingine vya siasa na kupokea ilanmi zao kwa moyo mkunjufu.
Alisema hayo katika hotuba yake baada ya kuapishwa mjini Dodoma jana.
Alisema kwamba ujenzi wa Taifa unategemea ushirikishwaji wa wadau wote, baada ya kumalizika kwa msimu wa uchaguzi.
Akishukuru wagombea wengine 17 wa nafasi ya Urais kwa kuonesha ukomavu wa kidemokrasia, Mhe. Rais alisisitiza kuwa mazungumzo huzaa mshikamano,akitaja falsafa ya Serikali yake ya Awamu ya Sita ya 4R's ambayo inaanza na Reconciliation (kuzungumza na kuelewana) na Resilience (kuvumiliana).
Mhe. Rais alisema kila sauti inathaminiwa na kusisitiza umuhimu wa ushirikishwaji. "Tutakuwa na nguvu zaidi pale kila sauti, chanya na hasi, zinaposikilizwa. kuheshimiwa na kuthaminiwa..."
Kauli hii inaweka wazi nia ya Serikali yake kupokea na kuzingatia mawazo na mapendekezo yanayotolewa na pande zote, ikiwemo yale yaliyokuwa yameainishwa katika ilani za vyama vingine vya siasa.
Wajibu wa Pamoja: Dkt. Samia aliwaeleza Watanzania kuwa demokrasia haipimwi na nani kashinda, bali kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa baada ya uchaguzi. Aliongeza kuwa jukumu la kuponya penye maumivu na kujenga mshikamano si la Serikali peke yake, bali ni kwa kila Chama cha Siasa, Jumuiya za Wananchi, na kila mwananchi




