NCCR MAGEUZI YAMPITISHA HAJI AMBARI HAMIS KUWA MGOMBEA URAIS 2025, WAWEKA WAZI MICHAKATO KUPATA WAGOMBEA WA UBUNGE NA UDIWANI
Na Neema Mpaka - Chama Cha NCCR Mageuzi kimewapitisha Haji Ambari khamis na Joseph Roman Selasini kuwa mgombea mwenza katika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ukaofanyika October mwaka huu.
Akizungumza mapema leo Mei 13, 2025 jijini Dar es salaam, katibu Mkuu wa Chama hicho. bi Evaline Wilbard Munisi amesema chama kimewapisha wagombea kwa upande wa Tanzania bara na kwa upande wa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Mgombea mwenza bado hawajapatikana hivyo chama kinaendelea na mchakato.
"Katika kikao cha halmashauri Kuu Taifa ya chama kilichofanyika Machi 30, mwaka huu chama kiliadhimia kwa kauli moja kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu kwa kusimamisha wagombea katika nafasi zote Tanzania bara na Zanzibar". Alisema Bi. Munisi
Alisema zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea katika nafasi mbalimbali za Urais, Ubunge na Udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao litaanza rsmi kuanzia Mei 31 hadi Juni 15, 2025 katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho
"Nitoe rai kwa Watanzania na mwanachama yeyote anayetamani kugombea nafasi kujitathmini kwa kuzingatia sifa za kuwa na maadili ya kitanzania kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama" Alisema Bi Munisi na kuongeza kuwa
"NCCR Mageuzi inamini kuwa wale wote wenye mapenzi mema kwa kujali UTU wetu, haki msingi za kila Mtanzania zitapatikana, kusimamia maslahi ya wengi dhidi ya wachache ndani na nje, pamoja na kusimamia na kutetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na chama hicho"
Katika hatua nyingine Bi Munisi ameiomba Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanya zoezi hilo la uchaguzi kuwa la Amani, huru na haki kama Rais alivyokwisha kutamka, tunaamini kwa kushirikiana, Elimu ya uraia itatolewa kwa wapiga kura, malalamiko yote ya hilo zoezi yatashughulikiwa kwa wakati muafaka nakwa haki.




