Breaking News

RASMI MIKOPO YA MABILIONI YA RAIS SAMIA KUANZA KUTOLEWA WIKI HII ILALA


Dar es salaam - Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema jumla ya sh. bilioni 18 za mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu zitaanza kutolewa wiki hii.

Amesema vikundi zaidi ya 900 vimejisajili na kuomba mikopo hiyo huku akiahidi kuhakikisha vikundi vyote vilivyo timiza vigezo na mashariti vitapata mikopo hiyo.

Ameyasema hayo ,mwishoni mwa wiki katika Kongamano la Jukwaa la Wanawake Kiuchumi la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mpogolo, alisema dirisha la utoaji mikopo hiyo litakapo funguliwa halitafungwa hivyo kuwataka wananchi wenye sifa kuendelea kuunda vikundi hivyo na kuvisajili kwa usahihi.
“Kiasi cha shilingi bilioni kumi n asana tayari zipo katika mzunguko. Kati awamu ya pili ya utoaji miko tunazo shilingi bilioni kumi na nane,” alieleza Mkuu huyo wa wilaya.

Aliwataka wanawake jijini Dar es Salaam, kuchangamkia fursa hiyo na kwamba watasimamia kikamilifu kuhakikisha wanasaidia vikundi kujisajili katika mfumo.

“Tutapita kila kata kila mtaa kutoa elimu ya kuanzisha na kusajili vikundi. Tunashukuru Jukwaa la Wanawake Kiuchumi limetusaidia kuwafikia wanawake wengi na tuwahakikishie, vikundi vyote vilivyo timiza vigezo na mashariti vitapata mkopo,” alisema Mpogolo.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam, Elihuruma Mabelya, alisema katika mikopo hiyo kiasi cha sh. bilioni 5 zimetengwa maalumu kwa vikundi vya wanawake.

Alisema, mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi ni sauti na nguzo muhimu ya uchumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Halmashauri yetu  itaendelea kutoa elimu ya mfumo mzuri wa upatikanaji mikopo ili wanufaika wapate tija ya kimaendeleo,”alisema.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Kiuchumi Wilaya ya Ilala, Rehema Sanga, aliwataka  wanawake wanaohitaji mikopo hiyo kumba kulingana na biashara zao na wasikubali kutumika kuomba mikopo nje ya biashara zao.

“Kwa mfano mtu ni mama lishe anaomba mkopo akijitambulisha fundi wa kushona nguo. Anashindwa kuandika mchanganuo hivyo kukosa sifa. Tunataka mama lishe aandike kazi yake anayoifanya ili tukija kumkagua tukute akifanya.