SHEKHE PONDA ISSA PONDA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE KUPITIA ACT WAZALENDO
Dar es Salaam — Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, Shekhe Ponda Issa Ponda, leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Temeke katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Shekhe Ponda amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Jimbo la Temeke, Ndugu Mussa Bakary, katika ofisi za chama zilizopo ndani ya jimbo hilo.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Shekhe Ponda amesema dhamira yake ni kuwatumikia wananchi wa Temeke kwa uadilifu na kuwawakilisha kwa ufanisi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia sera za ACT Wazalendo.
Katibu wa Jimbo, Ndugu Mussa Bakary, alimpongeza Shekhe Ponda kwa kuchukua hatua hiyo na kuwataka wanachama wengine wenye nia ya kugombea kujitokeza mapema ili taratibu za ndani ya chama ziweze kufuatwa kwa wakati.
Mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ndani ya ACT Wazalendo unaendelea kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na chama hicho.






