RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA MWISHO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
Dodoma — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika leo Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni hatua ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025. Baraza hilo limejadili utekelezaji wa shughuli za serikali katika kipindi cha uongozi wa awamu ya sita pamoja na mipango ya kuhitimisha muhula wa sasa wa uongozi.
Tangu kuingia madarakani mwaka 2021, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imejikita katika mageuzi ya kiuchumi, uboreshaji wa huduma za kijamii, na kuimarisha miundombinu ya kitaifa.
Kikao hiki kimehitimisha mfululizo wa vikao muhimu vya serikali kabla ya kuelekea kwenye kampeni za kisiasa na hatimaye uchaguzi mkuu ambao utaunda serikali mpya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.




