TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA KUZINGATIA SHERIA - JAJI MWAMBEGELE
Dar es salaam - Tume Huri ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imezitaka Taasisi na Asasi za Kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Akizungumza mapema leo Julai 30, 2025, Mwenyekiti wa INEC Jaji (Rufani) Jacobs Mwambegele akifungua Mkutano wa Tume na Wawakilishi wa Taasisi na Asasi za Kiraia kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 jijini Dar es Salaam.
"Napenda kuwahakikishia kuwa, Tume inathamini sana uwepo wenu kwa vile ni sehemu ya mafanikio ya kile tulichokusudia kuzungumza siku ya leo," amesema Jaji (Rufani) Mambegele na kuongeza,
"Pili na kwa umuhimu, nawashukuru nyinyi Wawakilishi wa Taasisi na Asasi za Kiraia, kwa namna ambavyo mmekua mkitupatia ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya Tume ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,".
Alisema Tume itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa zaidi kutoa kwa Tasisi na Asasi hizo ambazo zitatumia nafasi zao kwa jamii kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
"Ikiwia ni pamoja na kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kidumu la Mpiga Kura, wajitokezi kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka," ameongeza Jaji (Rufani) Mwambegele.
Jaji (Rufani) Mambegele ametumia fursa hiyo kuwashukuru kwa mchango wao kwa namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na Tume kwa kuwafikishia wadau ambao ni wanachama wa majukwaa yao taarifa kuhusu michakato mbalimbali ya uchaguzi hususan zoezi lilokamilika hivi karibuni la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Hivyo amesema kuwa Tume inawatambua kama daraja linalounganisha Tume na wadau kwa njia ya elimu, lakini pia kama moja wapo ya wadau muhimu wa Uchaguzi.
Hivyo kutokana na ukweli huo, Tume imeona umuhimu wa kufanya kikao cha pamoja ili kupeana taarifa na kufahamishana kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kwamba kikako hicho kinatoa nafasi ya kubadilishana na kupena uzoefu wa utekelezaji wa shughuli za uchaguzi ili kuhakikisha wanaepusha dosari ambazo zinaweza kujitokeza na kuathiri utekelezaji wa shughuli za uchaguzi.
Amesema kuwa hadi sasa Tume imefanya maandalizi mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu, hata hivyo ameeleza ili zoezi hilo lifanikiwe kwa kiwango kikubwa linategemea ushirikiano wao wawakilishi wa Taasisi na Asasi hizo katika kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa zoezi hilo.
Amebainisha kuwa Tume inaamini wakishirikishwa vyema na wakapata uelewa wa kutosha kuhusu mchakato wa Uchaguzi itakuwa rahisi pia kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kupitia majukwaa yao washiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Julai 26, 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge katika Jumhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara mwaka 2025.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, utoaji wa Fomu utaanza Agosti 9, 2025 hadi Agosti 27, 2025 mwa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais na kuanzia Agosti 14, 2025 hadi Agosti 27, 2025 ni utoaji wa Fomu za wagombea Ubunge na Udiwani na uteuzi utafanyika Agosti 27, 2025.
Kwamba kipindi cha kampeni za uchaguzi kitaanza Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025 kwa Tanzania Bara na kuanzia Agosti 28, 2025 hadi 0ktoba 27, 2025 kwa upande wa Tanzania Zanzibar.



