Breaking News

JUDITH KAPINGA AIBUKA NA USIHINDI WA KISHINDO JIMBO LA MBINGA VIJIJINI

Katika mchakato wa mchujo wa kisiasa uliofanyika Jimbo la Mbinga Vijijini, Judith Kapinga ameibuka mshindi kwa kishindo kikubwa baada ya kujizolea kura 12,975, akiacha wapinzani wake kwa tofauti kubwa ya kura.

Katika mchanato huo Judith Kapinga amewaacha mbali washindani wake akiwemo Benaya Kapinga aliyeshika nafasi ya pili kwa kura 1,292, na James Mapunda aliyepata 416. Wengine waliokuwa kwenye kinyang'anyiro hicho ni Allen Mhagama (133), CPA Martin (80) na Philimon Nkolela aliyepata kura 45 pekee.

Matokeo haya yanaashiria uungwaji mkono mkubwa kwa Judith Kapinga kutoka kwa wananchi wa Mbinga Vijijini, na kuweka wazi mwelekeo wa kisiasa wa jimbo hilo kuelekea uchaguzi mkuu ujao.