MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA: MTANDAO WA BARABARA WAFIKIA KILOMETA 144,429.77 KUTOKA KILOMETA 108,946.19 ZA MWAKA 2020.
Mtandao wa barabara nchini umeongezeka kwa kasi kubwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ukifikia kilomita 144,429.77 kutoka kilomita 108,946.19 zilizokuwepo mwaka 2020.
Katika kipindi hicho, ujenzi wa barabara za changarawe umeimarika kutoka kilomita 24,493 hadi 44,372.21, sawa na ongezeko la asilimia 81.16. Vilevile, barabara za vijijini na mijini zilizojengwa kwa kiwango cha lami zimeongezeka kutoka kilomita 2,025 hadi 3,467.30, ongezeko la asilimia 71.22