TANESCO YAZINDUA MFUMO WA KUPOKEA TAARIFA ZA SIRI.
Dar es salaam - Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) umezindua Mfumo wa kupokea taarifa za siri (Whistleblower portal) ambapo mfumo huo unaenda kurahisisha upokeaji wa taarifa kutoka kwa wananchi
Akizungumza Jijini Dar es salaam na wanahabari Kaimu mkurugenzi wa mawasiliano na huduma kwa wateja TANESCO Bi Irene Gowele amesema kwa muda mrefu shirika letu la Tanesco limekuwa likipata changamoto mbalimbali ambazo zinakwamishwa kwenye utoaji wa huduma endelevu ya umeme vikiwemo wizi, uharibifu wa miundombinu ya umeme,na vitendo vya rushwa kutoka kwa baadhi ya watumishi wa shirika hilo.
Mfumo huu mpya ni hatua muhimu ya kimageuzi katika utendaji kazi wa shirika la umeme TANESCO ambao unaenda kudhibiti uhalifu, uwajibikaji na ulindaji wa taarifa dhidi ya vitisho na kuongeza uaminifu wa umma wa shirika.
Aidha mtoa Taarifa ataelekezwa kwenye hatua stahiki huku taarifa hizo zikichukuliwa kwa siri kupitia mfumo huo hivyo sisi kama shirika tutashirikiana kwenye taarifa zote ambazo zitapelekwa na kutunzwa kwa siri na kushughulikiwa."Amesema Bi Gowele".
Sanjari na hayo Shirika la umeme Tanzania TANESCO linatoa wito kwa wananchi wote nchini kushiriki kikamilifu kwa kutumia mfumo huo ili kuweza kusaidia kulinda rasilimali na maslahi ya shirika na Taifa kwa ujumla.
"Kuna njia mbili ambazo zitatumika katika kuwasilisha taarifa hizo ambazo ni kupitia Tovuti ya TANESCO WWW.tanesco.co.tz ambapo unatakiwa kubonyeza kiungo cha (Whistleblowerportal) na utaweza kujaza fomu salama ya kutoa taarifa hiyo. ,kupiga simu ya bila malipo :Namba 180 kisha unabonyeza namba mbili na utaweza kuzungumza na watoa huduma wetu.
Vilevile katika kuendelea na kampeni yetu ya nchi nzima ya lipa deni tukuhudumie shirika linaendelea na kampeni hiyo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati kwenye maeneo yao husika.





