INEC NA VYAMA VYA SIASA WAKUBALIANA KUBADILI RATIBA YA KAMPENI YA UCHAGUZI 2025
Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndugu Adam Mkina, leo ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa. Kikao hicho kililenga kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
Mikutano hiyo, ambayo ilianza tarehe 28 Agosti, 2025, inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025, kwa Tanzania Bara. Kwa upande wa Zanzibar, mikutano hiyo itaendelea hadi tarehe 27 Oktoba, 2025, ili kupisha kura ya mapema itakayofanyika tarehe 28 Oktoba, 2025.
Uchaguzi Mkuu utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, ambapo wananchi watapewa fursa ya kuchagua viongozi wao. Kauli mbiu ya uchaguzi huu ni “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”, ikihimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.









