Breaking News

MECIRA WATOA WITO KWA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NA UHURU WAKUTOA MAONI

Dar es salaam - Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Raslimali na Taarifa (MECIRA) wametoa ushauri Watanzania kuendelea kudumisha amani, mshikamano wa Kitaifa na maelewano ya kijamii pamoja na kusisitiza umuhimu wa kutumia uhuru wa kutoa maoni na uwajibikaji

Akizungumza mapema leo desemaba 17, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa MECIRA bwana Habibu Mchange amessisitiza kwamba amani ya Tanzania ni tunu adhimu na muhimu inayopaswa kulinda na kila mwananchi.

"Tutaendelea kutumia njia za kiraia,kidiplomasia na kisheria kuhakikisha kuwa Tanzania inalindwa dhidi ya vurugu, propaganda hatarishi na miigawanyiko ya kijamii", alisema Mchange

Aidha, amesema kuwa uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kikatiba,lakinuto unapaswa kutumika na kuzingatia misingi ya maadili,Sheria nhout maslahi ya Taifa

Hata hivyo, ametoa wito kwa uongozi wa Kenye kuttumia njia ya amani yaani mazungumzo na mifumo ya kisheria katika kushughulikia changamoto zilizopo.

"Tunasisitiza umuhimu wa kuheshimu demokrasia,haki za binadamu na utawala wa Sheria kama nguzo kuu za kudumisha amani",