Breaking News

SALIM BIMAN AWAONGOZA WANACHAMA ACT-WAZALENDO MAZISHI BI. SITI YUSOUF

Zanzibar, Katibu wa Habari na Uenezi wa Chama cha ACT-WAZALENDO Salim Biman amewaongoza viongozi mbalimbali wa chama hicho visiwani Zanzibar kuusindikiza mwili wa marehemu Bi. Siti Yusouf Naim, aliyekuwa mke wa Naibu Katibu Mkuu wa chama Zanzibar, Omar Ali Shehe, hadi makaburi ya mwanakwerekwe.

Maziko ya marehemu huyo yamefanyika leo Asubuhi katika Makaburi hayo, ambapo amestiriwa huyo, viongozi wa chama, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wengi walijitokeza kushiriki katika ibada hiyo ya mazishi.
Akizungumza kwa niaba ya chama, Biman alitoa pole kwa familia ya marehemu, akiwataka waumini kuendelea kumuombea Dua marehemu pamoja na kuwapa moyo wafiwa katika kipindi hiki kigumu.

Marehemu Bi. Siti Yusouf Naim ameacha pengo kubwa kwa familia yake, ndugu na jamaa, huku chama cha ACT-WAZALENDO kikieleza kuguswa kwake na msiba huo na kusisitiza mshikamano wakati wa majonzi.