MBWENI WACHANGISHANA KUJENGA OFISI YA MTAA
Pichani ni Jengo la serikali ya mtaa wa Mbweni Malindi Estate ambalo wananchi wameamua kichangia ili kumalizia. Picha na Deusdema Chuwa
Na Mwandishi wetu - Baada ya serikali kutoa shilingi milioni 10 kwa ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mbweni Malindi Estate mkoani Dar es Salaam,baadhi ya wananchi wameamua kuunga mkono azma hiyo ili kukamilisha ujenzi uliosuasua kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa mtaa huo bibi Celina Mkony alieleza juzi kwamba wananchi kadha wameonesha uzalendo kwa kuchanga zaidi ya shiingi milioni mbili kuendeeza ujenzi huo.
Imeelezwa kwamba kati ya makada walioshupalia kuhamasisha ujenzi ni bwana Gaston Francis aliyetoa milioni moja na kuahidi kuleta baadhi ya vifaa, diwani wa kata ya Mbweni mstahiki Abdulkadry Mgheni aliyechangia laki tano na mwenyekiti mwenyewe naye limwaka laki tano,huku mwenyekiti mstaafu Bwana Clement Mshana akiweka laki moja.
Moyo huo wa kujitolea katika masuala ya maendeleo chanya ya taifa ulisisitizwa na diwani Abdullkadry ambaye alishauri viongozi wawe mstari wa mbele kuonesha wananchi njia za kushiriki miradi mbali mbali.




