PAPA: SINA HOFU NA TRUMP LICHA YA 'KUMSHAMBULIA' VIKALI
Papa Leo amesema hana "hofu yoyote" dhidi ya utawala wa Rais Donald Trump na ataendelea kutoa msimamo wake wa kupinga vita, kufuatia mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa Rais huyo wa Marekani kuhusu msimamo wake juu ya mzozo wa Iran.
Trump alimshutumu Papa huyo kwa kumuita "dhaifu katika kukabiliana na uhalifu na kwamba anamtazamo mbaya juu ya sera za nje" kupitia mtandao wake wa Truth Social, na baadaye kuwaambia waandishi wa habari kuwa yeye "si shabiki mkubwa wa Papa huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa njiani kuelekea Algeria katika ziara yake barani Afrika, Papa Leo amesema hataki kuingia kwenye mabishano na Trump, lakini ataendelea kusisitiza ujumbe wa amani.
Papa huyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa vita vya Iran, akielezea tishio la Trump la kuangamiza ustaarabu wa Iran kuwa "halikubaliki" na kwamba linavunja sheria za kimataifa huku akimtaka kutafuta njia ya kumaliza mzozo huo kwa amani.
Chanzo: BBC




