Breaking News

HAPI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Ally Salum Hapi (MNEC) ameongoza kikao cha kawaida cha kamati tendaji cha Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba iliyopo Kariakoo, Jijini Dar Es Salaam.