WAZIRI KATAMBI: ZUIO LA MIKUTANO YA HADHARA LINALENGA KULINDA USALAAMA, SIO KUZUIA DEMOKRASIA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema kuwa zuio la mikutano ya hadhara halilengi kukiuka misingi ya demokrasia nchini, bali ni hatua ya kuimarisha ulinzi na usalama. Amesisitiza kuwa demokrasia isiyokuwa na mipaka inaweza kusababisha fujo na kuhatarisha amani ya taifa.
Katambi ametoa kauli hiyo leo, Juni 29, 2026, wakati wa mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Akieleza msimamo wa Serikali, Waziri huyo alikumbusha kuwa Juni 26, 2026, alipokuwa akichangia bungeni jijini Dodoma, alieleza kuwa Serikali imepokea taarifa za baadhi ya watu wanaodaiwa kuhamasisha vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Amesisitiza kuwa Serikali haitawafumbia macho watu au makundi yoyote yatakayojihusisha na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na usalama wa nchi.




