Breaking News

MWENGE WAPONGEZA UWEKEZAJI WA HANNY G, WAENDELEA KUCHOCHEA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Mkurugenzi wa kampuni ya Hanny G Investment Hanny akiwa ameshika mwenge wa uhuru mara baada ya kuzindua kiwanda Hanny G Investment Co. Ltd kinachozalisha Jiko Poa na Kuni Poa (Briquettes), kilichopo Kijiji cha Kiseriani, Kata ya Mlangarini, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Meneja masoko wa kiwanda hicho Zera Negro akiwa ameshika mwengewa uhuru mara baada ya kuzindua kiwanda Hanny G Investment Co. Ltd kinachozalisha Jiko Poa na Kuni Poa (Briquettes), kilichopo Kijiji cha Kiseriani, Kata ya Mlangarini, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang'onda akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha Hanny G Investment Co. Ltd kinachozalisha Jiko Poa na Kuni Poa (Briquettes), kilichopo Kijiji cha Kiseriani, Kata ya Mlangarini, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.



Na Woinde Shizza, Arusha - KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang'onda, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji yanayovutia wawekezaji wengi zaidi nchini, hatua inayochochea ukuaji wa uchumi, kuongeza uzalishaji na kufungua fursa za ajira kwa Watanzania.

Mwang'onda aliyasema hayo Julai 10, 2026 wakati akizindua Kiwanda cha Hanny G Investment Co. Ltd kinachozalisha Jiko Poa na Kuni Poa (Briquettes), kilichopo Kijiji cha Kiseriani, Kata ya Mlangarini, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Kiwanda hicho ni miongoni mwa miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2026 na kina thamani ya Shilingi bilioni 3.5.

Alisema uwekezaji unaofanyika nchini unaendelea kuwanufaisha wananchi kupitia ajira, uzalishaji wa bidhaa za ndani na ongezeko la pato la taifa, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili sekta binafsi iweze kukua na kuzalisha ajira zaidi, hususan kwa vijana. Aidha, aliutaja Mkoa wa Arusha kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kuvutia uwekezaji kutokana na mazingira mazuri ya biashara na ushirikiano uliopo kati ya Serikali na sekta binafsi.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja Masoko wa Hanny G Investment Ltd, Zera Negro Mkiwa, alisema kampuni hiyo ilianzishwa Juni 3, 2016 kwa lengo la kutoa suluhisho la nishati safi ya kupikia kupitia uzalishaji wa kuni poa, mkaa poa, majiko banifu, vifaa vya kupasha na kuhifadhi chakula pamoja na mashine za kuanika mazao kwa kutumia mabaki ya mazao ya kilimo badala ya miti.

Alisema mradi huo unalenga kupunguza ukataji wa miti, kuhifadhi mazingira, kuboresha afya za wananchi kwa kupunguza moshi unaotokana na matumizi ya nishati za asili, kuongeza ajira kwa wanawake na vijana pamoja na kuunga mkono utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Mkiwa alisema hadi sasa Hanny G Investment Ltd imewanufaisha zaidi ya wananchi 625,000 na kuhudumia taasisi zaidi ya 650 nchini, huku Mkoa wa Arusha pekee ukiwa na taasisi 86 zikiwemo shule, vyuo na magereza zinazotumia nishati safi inayozalishwa na kampuni hiyo.l
Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja Masoko wa Hanny G Investment Ltd, Zera Negro Mkiwa, alisema kampuni hiyo ilianzishwa Juni 3, 2016 kwa lengo la kutoa suluhisho la nishati safi ya kupikia kupitia uzalishaji wa kuni poa, mkaa poa, majiko banifu, vifaa vya kupasha na kuhifadhi chakula pamoja na mashine za kuanika mazao kwa kutumia mabaki ya mazao ya kilimo badala ya miti.

Alisema mradi huo unalenga kupunguza ukataji wa miti, kuhifadhi mazingira, kuboresha afya za wananchi kwa kupunguza moshi unaotokana na matumizi ya nishati za asili, kuongeza ajira kwa wanawake na vijana pamoja na kuunga mkono utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Mkiwa alisema hadi sasa Hanny G Investment Ltd imewanufaisha zaidi ya wananchi 625,000 na kuhudumia taasisi zaidi ya 650 nchini, huku Mkoa wa Arusha pekee ukiwa na taasisi 86 zikiwemo shule, vyuo na magereza zinazotumia nishati safi inayozalishwa na kampuni hiyo.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo imechangia kuokoa zaidi ya miti milioni moja isikatwe, kuzalisha zaidi ya ajira 100 na kuwawezesha wakulima zaidi ya 2,000 kuuza mabaki ya mazao yanayotumika kama malighafi ya uzalishaji wa briquettes. Pia, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeipa kampuni kandarasi ya Shilingi bilioni 1.48 ya kujenga miundombinu ya nishati safi katika shule za sekondari 53 nchini.

Akihitimisha, Mkiwa alisema mafanikio ya Hanny G Investment Ltd yamechangiwa na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa kampuni itaendelea kuwekeza katika ubunifu na upanuzi wa huduma ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata nishati safi, salama, nafuu na rafiki kwa mazingira.