SPIKA ZUNGU AKUTANA NA KATIBU MKUU WA TEC, WAZUNGUMZA KUHUSU AMANI NA UMOJA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), leo Julai 6, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, katika Makao Makuu ya TEC yaliyopo Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya kitaifa, yakiwemo umuhimu wa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano nchini kama nguzo muhimu za maendeleo na ustawi wa Taifa.
Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEC, ambapo pande zote zimesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuendeleza utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania.








