WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA ELIMU YA VIPIMO KATIKA BANDA LA WMA SABASABA
Dar es Salaam, Julai 8, 2026 – Wakala wa Vipimo (WMA) umeendelea kutoa elimu kuhusu huduma za vipimo kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaotembelea Banda lake katika siku ya 11 ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).
Mbali na elimu hiyo, WMA pia inaendelea kutoa zawadi mbalimbali zenye nembo na jumbe za taasisi hiyo kwa wageni wanaotembelea banda hilo, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uelewa kuhusu umuhimu wa vipimo sahihi katika biashara na huduma.
Viongozi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali wameendelea kutembelea banda hilo kupata elimu na kufahamu majukumu ya Wakala wa Vipimo katika kulinda maslahi ya walaji na wafanyabiashara kupitia matumizi ya vipimo vinavyokidhi viwango.
WMA imewahimiza wananchi ambao bado hawajafika kutembelea banda lake katika Maonesho ya SabaSaba ili kupata elimu, huduma mbalimbali pamoja na fursa ya kujishindia zawadi.






