Breaking News

ASKOFU KESHOMSHAHARA AWATAKA VIJANA KUKUBALI CHANGAMOTO ZA MAISHA

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Dk Abednego Keshomshahara amewataka vijana kuamka, kutumia akili, vipawa na fursa walizonazo kukabiliana na changamoto za maisha na kuwa nuru katika jamii. 

Aliyasema hayo wakati akihubiri katika Sikukuu ya Vijana na Askofu 2026, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mwokozi Kengere Tatu Bukoba, ikiwa na kaulimbiu “Ondoka, Uangaze” kutoka Isaya 60:1. 

Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano ya vijana yaliyoanzia KKKT Nyumba ya Vijana Bukoba na kuelekea Kanisa Kuu ambako vijana walipokelewana Dk Keshomshahara aliyekuwa mgeni rasmi katika sikukuu hiyo. 

Katika mahubiri yake, Askofu alisema Mungu anahitaji kizazi cha vijana wenye mwelekeo, bidii, matumaini na uwezo wa kufanya maamuzi yanayojenga maisha yao na jamii. kutumia mitandao ya kijamii kwa kujenga jamii na kumtukuza Mungu, huku wakiwa makini na mafundisho potofu na kujenga imani yao katika neno la Mungu na maombi. 

Akirejea Mathayo 5:14 inayosema “Ninyi ni nuru ya ulimwengu,” askofu alisema vijana wanapaswa kuwa mifano Katika maadhimisho hayo, Dk Keshomshahara alizindua rasmi Akaunti ya Vijana ya KKKT–DKMG, hatua inayolenga kuimarisha huduma, mafunzo, uinjilisti, miradi ya maendeleo na programu mbalimbali za kuwawezesha vijana. 

Akisoma risala ya vijana kwa Askofu, Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana Dayosisi, Simon Samwel alisema vijana ni sehemu muhimu ya kanisa la sasa na la baadaye na wameahidi kushiriki kikamilifu katika ibada, uinjilisti, huduma za kijamii, elimu ya biblia na shughuli za maendeleo. 

Vijana pia waliahidi kuwa na hofu ya Mungu, umoja, nidhamu, bidii katika elimu na kazi, kushiriki katika huduma za kanisa na kutumia vipawa vyao kwa utukufu wa Mungu, huku wakilenga kuwa mifano mizuri katika familia, kanisa na jamii. 

Alisema vijana wanapaswa kuondoka katika usingizi wa kiroho, uvivu, hofu na kukata tamaa na badala yake kuamka na kutumia fursa zilizopo katika elimu, biashara, teknolojia, kilimo, sanaa na maeneo mengine. Aidha, aliwataka vijana kujikubali na kuacha kujilinganisha na wengine, hasa kupitia mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa kila kijana ana nafasi na kusudi lake mbele za Mungu. Aliwahimiza vijana