TMA YATOA UTABIRI WA MVUA ZA MSIMU NOVEMBA 2026 HADI APRIL 2027
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu wa Novemba 2026 hadi Aprili 2027 kwa mikoa 14 nchini, ikiwemo Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Mbeya na Ruvuma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mikoa mingine iliyojumuishwa katika utabiri huo ni Songea, Iringa, Njombe, Morogoro Kusini, Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara.
Utabiri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Benedict Chang'a, ukiwa sehemu ya juhudi za kuziwezesha sekta mbalimbali na wananchi kwa ujumla kujiandaa na kupanga shughuli zao kulingana na matarajio ya hali ya hewa katika kipindi hicho.
TMA imeeleza kuwa utabiri huo wa mvua za msimu unahusu maeneo yaliyotajwa kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia Novemba 2026 hadi Aprili 2027.
Wakati huo huo, utabiri wa mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026 ulitolewa rasmi mwezi Agosti mwaka huu, ukihusisha mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kaskazini mwa Kigoma.
Mikoa mingine iliyoainishwa katika utabiri wa Vuli ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Utoaji wa utabiri wa mvua za misimu ni muhimu kwa maandalizi ya shughuli za kilimo, mifugo, usafiri na sekta nyingine zinazotegemea hali ya hewa.




