PROF. MBARAWA AONYA TPA KUPEANA KAZI KINDUGU
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA), kuhakikisha inayapatia ufumbuzi matato yanayoikabili mamlaka hiyo kwa hivi sasa.
Prof.Mbarawa
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na bodi hiyo kupitia Teknolijia ya video
toka mjini Dodoma na kubainisha kuwa TPA inakabiliwa na matatizo mengi ikiwa ni
pamoja na wafanyakazi kupeana ajira kindugu.
Pia Waaziri,
alitaja utendaji usiozingatia matokeo, na mifumo mibovu ya ukusanyaji mapato
hali inayosababisha utendaji usiozingatia ufanisi.
Kwa upande
wake Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Prof. Ignas Rubaratuka amemhakikishia waziri
Mbarawa kuwa bodi yake imejipanga kukabiliana na matatizo yote ya bandari
nchini ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa.
Na shehe
semtawa



