BALOZI MATINYI AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO ALGERIA, AFANYA MAZUNGUMZO KUIMARISHA USHIRIKIANO
Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf, jijini Algiers, leo tarehe 26 Mei, 2026.
Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika mazungumzo mafupi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf, mara baada ya kuwasilisha nakala za hati za utambulisho jijini Algiers, leo Mei 26, 2026. Mazungumzo hayo yalihusu kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Algeria.





