BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB YAIPIGA JEKI TANZANIA DOLA MILIONI 200
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki
hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali kiasi cha
shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kulia), akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi
wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa
mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi
kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), akipeana mkono na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB, Tania Kandiero,
alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, kwa
mazungumzo maalumu, akiwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic
Kacou, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa
serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Makamu
wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia)
ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali
mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn. Aliyeketi kushoto ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Kushoto) akibadilishana “Business Card” na Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki
hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifuatilia kwa
makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,
Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia
Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi
433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), (Katikati), akiwa
katika mazungumzo maalumu na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi yake
Jijini Dar es slaam, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa
Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
Kaimu
Kamisha Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta
Mtagwaba akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani), ambapo
Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akibadilishana “Business Card” na Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki
hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa katika mazungumzo
maalumu na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa
na Makamu
wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, aliyeambatana na Mkurugenzi
Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero, ambapo Benki hiyo
imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017,
kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto)
akizungumza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo
ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na Makamu
wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia)
ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali
mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
…………………………………………………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja-WFM
BENKI ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,
imeahidi kuchangia Dola Milioni 200, sawa na Shilingi 433.6b, kwenye
Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa Fedha
2016/2017.
Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa
Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu, Dkt.
Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es salaam
Makamu huyo wa Rais wa AfDB
aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Tania Kandiero, amesema
kuwa mchango huo umeongezeka kwa dola Milioni 50 ikilinganishwa na
Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo ilichangia Dola Milioni 150.
“Misaada na mikopo inayotolewa na Benki yetu kwa serikali ya Tanzania
imefikia Dola za Marekani 1.9b hivi sasa” Alieleza Dkt. Kacou
Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi
inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi kikubwa cha fedha
kutokana na mipango yake mahili ya maendeleo inayokidhi vigezo na
viwango vya taasisi hiyo. “Tuna malengo matano ambapo tunataka kuwekeza
katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula, kuiendeleza kiviwanda,
kuiunganisha na kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla” aliongeza Dkt.
Kacou
Amepongeza jitihada zinazochukuliwa
na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli,
kwa kusimamia vizuri nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kwamba
uamuzi huo utaharakisha maendeleo ya nchi. Akizungumza na ujumbe huo,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameshukuru uamuzi wa
Benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika Bajeti Kuu ya serikali
kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS).
Amesema kuwa serikali imedhamiria
kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
kimataifa (standard gauge), pamoja na kununua ngege tatu za abiria ili
kuboresha usafiri wa anga.
“Vilevile tumeamua katika Bajeti ya
mwaka huu kununua meli mpya itakayo tumika kutoa huduma Ziwa Viktoria na
kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na
nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa majini” Aliongeza Dkt.
Mpango.
Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika
kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, serikali imejipanga
kukuza sekta ya viwanda ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025. “Mpango huo utakwenda sambamba na kuboresha sekta ya
kilimo ili malighafi itakayozalishwa na wakulima, licha ya kuinua
uchumi wa wakulima wetu, lakini pia viwanda vitapata malighafi ya
kutosha” alisisitiza Dkt. Mpango
Amerejea msimamo wa serikali kuwa
haitakubali kupokea misaada inayoambatana na masharti magumu na isiyo na
tija kwa nchi na kwamba jitihada zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha
kuwa rasilimali zilizopo nchini zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili
ziweze kutumika kuleta maendeleo.
“Hatutakubali misaada isiyozingatia
vipaumbele vyetu na ile inayohatarisha uhuru wetu wa kujiamulia mambo
yetu wenyewe” alieleza Dkt. Mpango.Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali wa
kukusanya mapato yake ya ndani kwa kuwahimiza watu kulipa kodi na kubana
matumizi yasiyo ya lazima umeanza kuleta matunda na kuongeza pia
nidhamu ya matumizi ya pesa katika jamii.
Ameiahidi Benki hiyo ya maendeleo ya Afrika-AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.



