BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe
alipotembelea kukagua ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa
KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto)
akisalimiana na Wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe,
Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya
Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango
cha lami.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimbeba
mtoto aliyehudhuria kikao cha Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya
Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa
barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa
kwa kiwango cha lami.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akicheza na
wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe
waliokuwa na furaha mara baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa barabara
ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa
kiwango cha lami.
Muonekano wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Meneja
wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Iringa Bi. Elikael Manase
akitoa maelezo kwa Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa kuhusu athari ya mmomonyoko wa ardhi unavyoathiri sehemu
ambayo Mkongo wa Taifa umepita eneo la Lukumburu Mkoani Njombe.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mbele)
akitoka kukagua eneo lililoathirika na mmomonyoko wa ardhi eneo la
Lukumburu Mkoani Njombe.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati alipotembelea
kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe.
Wafanyakazi
wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
wakimsikiliza Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea
kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe.
Wakazi
wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe
wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa wakati alipotoa taarifa ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete
yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
……………………………………………………………………………………………
Serikali imesema ipo katika hatua
za mwisho kuanza ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete kwa kiwango cha
lami yenye urefu wa KM 109.4 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Njombe ili
kurahisisha huduma ya usafiri wa barabara kwa wakazi wa mikoa hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo mkoani Njombe wakati
akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, kata ya Ulembwe, wilaya ya
Wanging’ombe mara baada ya kukagua barabara hiyo.
Profesa Mbarawa amesema kuwa
Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo imetenga kiasi cha
sh.bilioni 19 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya
ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
“Tumejipanga na tuna nia dhabiti
kuhakikisha barabara hii tutaijenga kwa kiwango cha lami na katika
kuharakisha kazi hii tutatafuta makandarasi wawili ili ujenzi huu
ukamilike kwa haraka”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa
amewataka wananchi kushirikiana na Makandarasi watakapoanza ujenzi huo
ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kulete tija kwa wananchi wa
Mikoa ya kanda ya kati.
Amesema kuwa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS) Mkoa wa Njombe upo katika hatua za kutangaza zabuni
ili kupata Makandarasi wenye uwezo wa kujenga barabara hiyo kwa
kuzingatia viwango kulingana na mkataba.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa
Njombe Eng. Yusuph Mazana amesema kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa
kina wa barabara ya Njombe-Makaete yenye urefu wa KM 109.4 kwa ajili ya
ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umekamilika na Mhandisi
mshauri M/s Crown Teach Consult Ltd ameshawasilisha taarifa ya usanifu
wa kina.
“Tumepokea taarifa ya usanifu wa
kina kutoka kwa Mhandisi Mshauri hivyo tunahaidi kusimamia utekelezaji
wa mradi huu kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa mkoa wa Njombe na
mikoa jirani”,amesisitiza Eng. Mazana.
Waziri Prof. Mbarawa ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara hiyo Mkoani Njombe.



